Baraza la Sanaa la Taifa [BASATA], Limefunguka na
kukili kuwa kuna baadhi ya wasanii wa njee ya nchi wanaokuja nchini na kufanya
biashara ya Ngono, katika kumbi mbali mbali za starehe hapa jijini DSM,
wakisingizia wanakuja kufanya shughuli za sanaa...........
Hali hiyo imebainika baada ya Idara ya uhamiaji
kubaini kuwa kuna baadhi ya maofisa wa idara hiyo wanaodaiwa kupokea rushwa na
kuusaidia mtandao unaojihusisha na biashara hiyo.
Wengi wao wanatokea katika mataifa ya India, Nepal, Pakistan na Bangladesh. Wasichana hao mbali na
kujihusisha na biashara ya ngono hujihusisha pia na biashara haramu ya
binadamu.
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Abbas Irovya alitoa
taarifa ya kuwepo kwa biashara hiyo inayokiuka masharti ya vibali vya kuingia
nchini na kujihusisha na biashara ya ngono.
0 maoni:
Post a Comment