MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

MALAYSIA YAZIDISHA KASI YA KUITAFUTA NDEGE ILIYOTOWEKA.



 
Shughuli ya kutafuta ndege ya abiria ya Malaysia imeendelea kushika kasi baada ya kuwepo kwa hali ya suitofahamu na wasiwasi mwingi kutoka kwa ndugu za watu waliopotea wakiwa katika ndege hiyo................


Mamlaka nchini Malaysia zinasema wameongeza mipaka ya eneo la utafutaji, mara mbili Zaidi, huku China ikiwa imepeleka mitambo 10 ya satelaiti kwa ajili ya kusaidia kutafuta ndege hiyo.

Mkuu wa Idara ya anga Azharuddin AbdulRahman amewaambia waandishi wa habari kuwa eneo la kusaka ndege hiyo limeongezeka mara mbili kutoka maili 50 za baharini kunakosemekana ndege ilipotelea mpaka maili 100.

Ndege iliyokua imebeba watu 239 ilipotea bila kutoa taarifa yeyote na hakuna dalili yeyote mpaka sasa ya kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment