Raia wa nchini Somalia aliyecheza Film ya Captain
Philips, amepata shavu jipya baada ya kuonekana kwenye Film ya Captain Philips,
sasa atacheza Movie mpya nchini Afrika Kusini............
Barkhad Abdi ambaye mbali na mkwanja mrefu alioingiza
kupitia filamu ya Captain Phillips aliyoigiza kama mkuu wa haramia, aliwahi
kulipwa kiasi cha dola 65,000 baada ya kuwekwa kwenye orodha ya waigizaji
wanaowania tuzo za Oscar, bado ameonekana akiweweseka kiuchumi japo hajafikia
hali ile aliyotoka nayo Somalia.
Abdi ameweza kupata nafasi nyingine ya kuigiza katika
filamu kubwa kama mwanariadha mkongwe wa Afrika Kusini, Willie Mtolo ambayo inaitwa ‘The Place That Hits The Sun,
na huenda hiyo ikamuokoa kutoka kwenye msoto.
0 maoni:
Post a Comment