Rais Jakaya Kikwete leo
anatarajiwa kuzindua rasmi shughuli za bunge la kitaifa kuhusu marekebisho ya
katiba mjini Dodoma
katika hatua itakayoanzisha rasmi mjadala wa kitaifa kuhusu marekebisho hayo...........
Bunge hilo maalum la katiba limepewa kati ya siku 70 hadi 90 kujadili rasimu ya katiba na kisha kuifanyia marekebisho kabla ya kura ya maamuzi.
Kuna ripoti kwamba baadhi ya wajumbe kutoka upinzani na mashirika ya kiraia yanapanga kuvuruga shughuli hiyo ya uzinduzi.
Suala la hotuba ya Rais Kikwete limekuwa sehemu ya mjadala katika Bunge hilo kutokana na baadhi ya wajumbe kuhoji sababu za Jaji Warioba kuwasilisha Rasimu kabla ya Rais kuzindua Bunge kwa mujibu wa kanuni
0 maoni:
Post a Comment