MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

WAZANZIBAR KURUDI KWAO, MUUNGANO WA MKATABA, MAKAMU WA RAIS ZNZ, AMEFUNGUKA ZAIDI.



 Screen Shot 2014-03-28 at 3.12.21 AM
Kama ulisikia stori za kikundi flani au mtu flani kusikika akisema ameagizwa kufikisha taarifa kwamba hawautaki muungano… hii post ni mali yako.............


Balozi Seif Ali Idd ambae ni makamu wa pili wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar amezungumza na vyombo vya habari March 27 2014 na kusema  ‘wanaosema Wanzanzibari wote hawataki muungano bali wanataka mkataba hii ni kauli potofu, alikutana nao wapi Wazanzibari hao wakasema hivyo? Wazanzibari wako zaidi ya milioni moja na laki tatu… alifanya nao wapi mkutano huo na kukubaliana kwamba uwepo muungano wa mkataba? ni vyema angesema yeye na kundi lake ndio wanataka mkataba’

Aliendelea kwa kusema kuwa ‘kitendo cha baadhi ya viongozi hao wa kisiasa kuwataka Wazanzibari wanaofanya shughuli zao na kuishi Tanzania bara waache shughuli zao na kurudi Znz, nia yao ni kuwatenganisha… kama haufahamu kiasili Wazanzibari wengi asili yao ni Tanzania bara’




‘Leo Zanzibar hakuna hata Mzanzibari mmoja atakaefatilia asili yake na kujikuta haihusu Tanzania bara hivyo swala la kuasisiwa kwa muungano mwaka April 1964 ilikua ni kurasimishwa tu lakini muungano huu ulikuepo tayari miongoni mwa Wananchi wa pande hizi mbili, serikali ya Mapinduzi Zanzibar iko macho na yeyote atakaejaribu kuleta fujo atashughulikiwa kikamilifu’

Baada ya Waandishi kuhoji uwepo wa katiba mpya ya Zanzibar Balozi amejibu ‘Ofcourse Zanzibar ni nchi kwa sababu ni moja ya nchi zilizofanya muungano…… isipokua tofauti ni moja tu ambayo wengi hawaielewi… Zanzibar haina utaifa, Tanganyika na Zanzibar zote zimechukuliwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwani ukienda nchi za nje huwa unakuta ubalozi wa Znz? no haupo’





Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment