Habari zilizotangazwa juu ya mawasiliano ya mwisho
kati ya wafanyakazi wa Feri iliyozama Korea Kusini na maafisa wa kudumisha
usalama baharini zinaonyesha kuwa kulitokea hali ya wasiwasi kabla ya mkasa
huo, ambayo huenda ilichangia pakubwa vifo vya abiria wengi katika feri hiyo............
Taarifa hiyo mpya imetolewa jana alasiri wakati ambapo
imethibitishwa kuwa maiti 62 zimepatikana kwenye mabaki ya feri hiyo, na
kufanya idadi ya watu waliothibitishwa kufariki kufikia 58. Zaidi ya watu 240
hawajulikani waliko hivi sasa.
Jamii za watu ambao hawakuwa wamepatikana walifanya
maombi ya Pasaka Jumapili katika chumba cha kufanyia mazoezi katika eneo la
Jindo, ambako mamia ya watu wamekusanyika tangu feri hiyo kupinduka wakisubiri
habari kuwahusu wapendwa wao.
Mama mmoja alisema kuwa watoto waliofariki walikuwa
wakitunzwa vizuri.
"Naamini watoto hao wako mbinguni na Mwenyezi
Mungu aliyefufuka. Naamini Naamini mimi," mama huyo alisema.
Jung Maria, mwanamke aliyejitolea kuzisaidia familia
za walioathirika, alisema kuwa jamaa za watu wasiojulikana waliko wanapaswa
kusikia kilichotokea kwa njia moja au nyingine.
"ikiwa wamefariki, tunapaswa kupata miili yao haraka iwezekanavyo.
Na iwapo kutatokea muujiza basi turejeshewe watoto hao upesi pia, alisema
mfanyakazi huyo wa kujitolea
Idadi kubwa ya abiria katika meli hiyo walikuwa
wanafunzi wa shule ya upili waliokuwa wakienda kwenye mojawapo wa kisiwa
kubarizi. Hadi kufikia sasa kumekuwa kungali kuna ubishi mkubwa iwapo nahodha
mwenyewe alikuwa ameshikilia sukani.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment