Marekani inasema imesikitishwa na makubaliano kati ya
makundi makuu Palestina ya kuiunda serikali ya Umoja...............
Imeoya huenda hatua hiyo ikatatiza zaidi jitihada za
amani. Uamuzi huo unalijumuisha kundi lenye msimamo kali za kidini, Hamas,
unaliotawala eneo la Gaza na limetajwa na
Marekani na Israeli kama kundi la kigaidi.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Marekani Jen
Psaki amesema wakati wa kutangaza uamuzi hduo ndio unaotia wasiwasi.
Tangazo hilo
limefanywa wakati ambapo Marekani ilikuwa ikijitahidi kushawishi Israil na
Wapalestina kukubali kuendelea kufanya mashauriano ya amani ambayo hadi kufikia
sasa hayajazaa matunda yo yote.
Bi Psaki amesema mapatano kati ya Wapalestina
yatavuruga vibaya sana juhudi hizo na akatangaza
kuwa itakuwa vigumu kwa Israil kufanya mashauriano nakundi ambalo haliamini
kuwa Israili ina haki ya kuwepo kama taifa;
jinsi wanavyoamini wanachama wa Hamas.
Alisema Serikali ya Marekani itaendelea kuchunguza kwa
makili hatua zinazochukuliwa kuhusiana na uamuzi huo na Wapalestina siku na
hata masaa yanayokuja.
Wamarekani na mataifa washirika wake wamesisistiza
kuwa muda mrefu kuwa taifa lo lote la Wapalastina inapaswa kuwa lile
linaloshutumua vita, litambue Israil na kukubalia mapatano yote yanayohusisha
taifa hilo la
Wayahudi.
Wapalestina wanasisitiza kuwa umoja wao utampa uhalali
zaidi Rais Mahmoud Abbas, kufanya mashauriano kwa niaba yao
kwa sababu atakuwa akiwakilisha Wapalestina wote na wala sio baadhi yao tu.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment