Mshiriki wa shindano la Big Brother Africa ‘The
Chase’, Ammy Nando ameweka wazi kuwa alikuwa mmoja kati ya waathirika wa dawa
za kulevya.............
Akiongea katika kipindi cha Hatua Tatu ha 100.5 Times
Fm, Nando amesema alikuwa anatumia dawa hizo za kulevya kwa muda mrefu na
kwamba hadi leno ni wiki ya 16 tangu afanye uamuzi wa kuacha.
Akizungumzia sababu zilizompelekea kutumia dawa za
kulevya, amesema ujana na maisha ya starehe aliyoishi vilichochea.
“Sababu ya kuingia huko, ni ujana tu mwanangu…unajua
ujana ni maji ya moto kama watu wanavyosema.
Na pee pressure na watu niokuwa nao wakati ule, na life nililoishi mimi...ni
yale maisha ya kujiachia.” Amesema Nando.
Hata hivyo, Nando ameeleza kuwa ameachana na dawa za
kulevya (unga) lakini bado anatumia bangi kwa hivi sasa japo amepunguza idadi.
“kuhusu bangi…sisi tunaitaga stock, natumia moja au
mbili kwa siku.”
Ameongeza kuwa yeye ni mmoja kati ya watu wenye kibali
cha kuvuta bangi katika jimbo la California
kwa maelezo ya daktari kuwa anafanya hivyo kwa lengo la kuacha kutumia unga.
Kutoka Timesfm.
0 maoni:
Post a Comment