Inaripotiwa kuwa China
imetuma silaha zenye thamani ya dola milioni 38 nchini Sudan Kusini
licha ya nchi hiyo kukabiliwa na mzozo ambao huenda utaitumbukiza katika baa la
njaa................
Nyaraka zilizogunduliwa na wataalamu wa masuala ya ulinzi zinaonyesha kuwa makombora, bunduki za rashasha na risasi viliwasili nchini Sudan Kusini mwezi uliopita kupitia bandari ya Mombasa nchini Kenya.
Wanadiplomasia wanakadiria kuwa Sudan Kusini inatumia mamilioni ya dola kwa ulinzi.
Kwingineko, muungano wa ulaya umewawekea vikwazo viongozi na kupiga tanji mali ya wakuu wa kijeshi wa nchi hiyo kwa tuhuma za kukiuka makubaliano ya kusitisha vita ambayo yangeleta mazingira ya amani na kuziia mauaji ya maelfu ya wanachi.
0 maoni:
Post a Comment