Shirika la madaktari wasio na mipaka MSF limesema kuwa takriban watu
elfu arubaini wanaishi katika mazingira mabaya katika kambi moja ya umoja wa
mataifa nchini Sudan Kusini..............
Shirika hilo limesema kuwa maelfu ya raia wanaishi katika eneo lenye mafuriko yaliochanganyika na maji taka katika kambi ya Bentiu ambapo wamekimbilia hifadhi ili kukwepa vita kati ya vikosi vya serikali na waasi wa taifa hilo.
Limesema kuwa raia wengi katika kambi hiyo hawawezi kulala na hivyobasi husalia kusimama wakiwabeba wana wao.
MSF limesema kuwa mazingira hayo ni ukiukwaji wa utu wa kibinaadamu.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment