Rais wa Uchina, Xi Jingping, amewasili nchini India na kutoa
mwito wa ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili kwa manufaa ya maendeleo....................
Rais Xi Jinping, amesema kuwa nchi zote mbili ziko katika
hatua muhimu za mabadiliko na maendeleo. Amesifia faida za muungano na
ushirikiano wa mataifa hayo mawili.
Ziara hiyo inatazamia kuboresha uhusiano kati ya mataifa
huyo mawili ambayo kwa muda mrefu ulikuwa mmbovu.
Mwenyeji wake atakuwa Waziri Mkuu mpya wa India, Narendra
Modi, ambaye amewahi kutangaza wazi kuwa anapendelea uongozi wa uchina na kuwa
anatafuta njia ya kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo.
Wanatarajiwa kutia sahihi ushirikiano wa kibiashara wa
mabillioni ya madola katika uwekezaji wa China katika harakati za kuimarisha
uhusiano na Waziri Mkuu mpya wa India, Narendra Modi, licha ya mvutano wa
msingi kuhusu mpaka wao na ushindani wao wa ushawishi wa kikanda.
Rais
Xi amekutana na waziri mkuu wa Narendra Modi wa India
Mataifa hayo mawili ambayo yanazozania mpaka yanangangania
umashuhuri katika eneo lao na rasilmali za nishati.
Swala lingine linalotatanisha kati yao ni kuwa kiongozi wa
Tibet aliye uhamishoni, Dalai Lama, anaishi Kaskazini mwa India. Ameombwa
aahirishe ziara yake ya New Delhi ili isigongane na ile ya Bwana Xi.
Lakini shughuli za kibiashara kati ya mataifa hayo
zinaimarika kwa kuwa inatarajiwa kwamba Bwana Xi ataleta nchini India uekezaji
wa zaidi ya Dola Bilioni 100.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment