Wananchi
wa Indonesia wameanza kuadhimisha mwaka wa kumi tangu kutokea kwa tetemeko la
ardhi lililosababisha mawimbi makubwa katika bahari ya Hindi, tsunami na
kusababisha vifo vya watu zaidi ya watu laki mbili na elfu ishirini katika eneo
kubwa..............................
Umati
wa watu umekusanyika karibu na jengo la makumbusho la tsunami katika eneo la
Banda Aceh katika kisiwa cha Sumatra.
Mji
huo ulisambaratishwa kabisa na tetemeko kubwa la ardhi na mawimbi ya tsunami.
Makamu wa Rais wa Indonesia(Jusuf Kalla) anaongoza maadhimisho hayo na
atawashukuru wafanyakazi wa kujitolea katika eneo hilo na duniani kote kwa
kulisaidia eneo la Aceh kurejea katika hali ya kawaida baada ya mkasa huo.
0 maoni:
Post a Comment