Inaarifiwa
kuwa watu kama 30 waliuwawa katika mashambulio kwenye vijiji mashariki mwa
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo................
Taarifa
zinasema kuwa mashambulio hayo yalifanywa Jumamosi usiku kwenye vijiji karibu
na mji wa Beni ambako watu zaidi ya 250 wameuawa tangu mwezi Oktoba.
Wakuu
na mashirika ya raia yanawalaumu wapiganaji kutoka Uganda wa kundi la ADF,
lakini baadhi ya wadadisi wanasema hakuna ushahidi wa kutosha wa kuhusisha
kundi hilo.
Mwandishi
mmoja wa habari katika eneo hilo aliambia BBC kuwa waliofariki ni pamoja na
wanawake na watoto ambao walibururwa kutoka kwa nyumba zao na kukatwa katwa kwa
mapanga.
Alisema
haijulikani nani aliyefanmya mashambulizi hayo, ingawa maafisa wakuu wamelaumu
kundi la waasi la Uganda la ADF.
Alisema
maelfu ya watu wameachwa bila makao kutokana na vurugu zinazoendelea na kwamba
wanahofia sana kurejea makwao.
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment