Ndege
ya mizigo iliyosheheni silaha za kivita imekamatwa katika uwanja wa ndege wa
Kano nchini Nigeria.......................
Licha
ya kukanusha awali, Urusi imesema inamiliki ndege ya mizigo iliyozuiwa katika
uwanja wa ndege wa Kano kaskazini mwa Nigeria baada ya kugunduliwa imebeba silaha
ambazo hazikuwa zimearifiwa.
Hata
hivyo, Msemaji wa Ubalozi wa Urusi nchini Nigeria, ambaye aliliambia Shirika la
Habari la Urusi TASS kwamba wanamiliki ndege hiyo, amesema silaha hizo ni za
kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa.
Kwa
mujibu wa Mwandishi wa habari wa BBC ndege hiyo bado inashikiliwa uwanjani
hapo.
Awali,
msemaji wa kikosi cha kulinda amani cha Ufaransa katika Jamhuri ya Afrika ya
kati aliiambia BBC kwamba hawafahamu chochote kuhusu helikopta mbili, magari ya
kijeshi na silaha nyingine zilizokuwa katika ndege hiyo.
Hata
hivyo baadaye alipiga simu kufuta usemo wake kwa kusema kuwa ndege hiyo ilikuwa
imebeba silaha kwa ajili ya wanajeshi wao, walioko katika kambi ya N’damena,
ambazo zitapelekwa baadaye Ufaransa.
Msemaji
wa Ubalozi wa Urusi mjini Abuja alisema pia ndege hiyo ni yao. Akitatanisha
taarifa aliyoitoa awali kwamba ndege hiyo si yao.
Kwa
nini Ufaransa inatumia ndege ya Urusi kubeba silaha zake? na kwa nini ilisimama
katika uwanja wa Kano, wakati ikiwa inaelekea nchi jirani ya Chad na hata
Cameroun ikitokea Afrika ya kati? Kwanini baadhi ya silaha hazikuorodheshwa
katika ndege hiyo kama zimebebwa?.
Hayo
ni maswali yalioulizwa pande zote.
Seriakli
ya Nigeria ambayo ndio muhusika mkuu wa tukio hilo, haijasema chochote.
Baadhi
ya wachambuzi wanasema Nigeria inamiliki silaha hizo ilizonunua katika soko
haramu. Wengine wanasema silaha hizo zilinunuliwa kutoka kwa waasi wa Seleka
katika Jamhuri ya Afrika ya kati, wakielezea kwanini ndege hiyo imeingia nchini
humo kutoka mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui.
Nigeria
imewekewa vikwazo vya silaha kutoka Marekani na nchi hiyo imekuwa ikiarifiwa
kutumia njia zisizo halali kupata silaha kwa ajili ya kupambana na wapiganaji
wa Boko haram.
Kutoka
BBC
0 maoni:
Post a Comment