Mahakama
nchini Ivory Coast imemhukumu aliyekuwa mke wa Rais wa nchi hiyo Laurent
Gbagbo, kifungo cha miaka 20 gerezani................
Simone Gbagbo
amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki
katika ghasia
zilizotokea baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2010 na 2011.
Simone Gbagbo
alikamatwa mwaka 2011 pamoja na mume wake, aliyekuwa rais wa nchi hiyo Laurent
Gbagbo, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika
mahakama ya uhalifu mjini The Hague Uholanzi.
Katika ghasia hizo watu
takriban elfu tatu walifariki dunia.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment