Waziri mkuu wa
Ufaransa,Manuel Valls, amesema kwamba watu wanaohusishwa na kundi la Islamic
State ambao walitekeleza shambulizi mjini Paris wiki iliyopita,ambalo
liligharimu uhai wa watu mia moja na ishirini na tisa,waliingia nchini humo kwa
mgongo wa sakata la uhamiaji barani ulaya na kuzamia nchini Ufaransa bila
kugundulika.
Ameyasema hayo wakati
alipokuwa anazungumza katika runinga ya taifa hilo na kwamba wahusika wengine
wa ugaidi walikuwemo katika nchi za Ufaransa na Ubelgiji mapema.
Waziri huyo aliongeza
kuwa haikufahamika mara moja kwamba kulikuwa na makundi ya namna hiyo kwa
ukubwa wake ,ama mshukiwa Salah Abdeslam, ambaye ndiye hasa kielelezo cha
mwanamume anayesakwa zaidi kimataifa na haikujulikana kama alikuwa Ubelgiji ama
Ufaransa.
CHANZO BBCSwahili
0 maoni:
Post a Comment