Utafiti ulioendeshwa
nchini Marekani unaonyesha raia wengi wa Mexico wanaondoka kwenye taifa hilo
kubwa zaidi ulimwenguni ukilinganisha na idadi ya wanaoingia nchini
humo,tofauti na hali ilivyokuwa nusu karne iliyopita.
Utafiti huo uliofanywa
na kituo cha utafiti cha Pew umeeleza kwamba katika kipindi cha miaka mitano
mfululizo mpaka kufikia mwaka wa jana, inakadiriwa Wamexico milioni moja wakiwa
na familia zao wameondoka nchini Marekani na kurejea nchini Mexico.
Katika kipindi kama
hicho,wa Mexico elfu moja na arobaini waliondoka nchini mwao kuelekea Marekani
kutafuta makazi bora.kituo hicho cha utafiti kinatanabahisha sababu kubwa ya
kurejea nyumbani kwa wa Mexico, ni ile hamu ya kutaka kuungana na familia zao.
Ripoti hii imetolewa
wakati huu ambapo wimbi la wahamiaji kuingia nchini humo likiwa limeongezeka
katika kampeni za urais nchini Marekani .
Mgombea mmoja kutoka
upande wa chama cha Republican , Donald Trump, ametoa wazo la kujengwa kwa
ukuta kati ya Mexico na Marekani kwa misingi ya kuzuia uhalifu unaofanywa na wa
Mexico pamoja na usafirishaji dawa za kulevya kutoka Mexico na kuziingiza
Marekani.
kutoka BBCSwahili.
0 maoni:
Post a Comment