Serikali ya Marekani
imetoa tahadhari ya kusafiri duniani kote kwa raia wake, ikiwaonya kuwepo kwa
ongezeko la tishio la kigaidi.
Tahadhari hiyo inasema
taarifa zilizopo hivi sasa zinaashiria kwamba makundi kama vile Islamic State,
al-Qaeda na Boko Haram wanaendelea
kupanga mashambulio katika maeneo tofauti.
Inawataka wasafiri kuwa
makini hasa wanapokuwa katika mikusanyiko ya watu au pindi wanapotumia usafiri
wa umma.
Hata hivyo, afisa
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ameiambia bbc kwamba hakuna sababu ya
kuamini kwamba raia wa Marekani ndio walengwa.
Mamilioni ya raia wa
marekani watasafiri wiki hii kwa ajili ya sikukuu ya kutoa shukrani siku ya
alhamisi.
kutoka BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment