Misururu mirefu
imeonekana kwenye vituo vya uuzaji mafuta nchini Nigeria,kutokana na sababu ya
kuwepo mgawanyiko baina ya serikali na waagizaji mafuta kutokana na kutolipwa
kwa ruzuku.
Serikali ya Nigeria
tayari ilikwisha idhinisha zaidi ya dola za kimarekani bilioni mbili kama
malipo ya malimbikizo ya nyuma,lakini Rais
Muhammadu Buhari amesisitiza kuwa
suala hilo liwasilishwe bungeni.
Utawala ulioondoka
madarakani nchini humo ulilipa ruzuku bila ya kuwashirikisha wabunge,lakini
rais Buhari ameahidi kupambana narushwa.
Inadaiwa kuwa waagizaji
hao wa mafuta wanadai kwamba madai yao ya ruzuku ya mafuta ni ndogo
ukilinganisha na faida wanayoipata.
Pamoja na kwamba ni
wazalishaji wakubwa wa mafuta,Nigeria inalazimika kuagiza mafuta nje ya nchi
hiyo karibu lita milioni arobaini za petroli kwa matumizi ya kila siku ya
madereva wake,huku ikiwa na viwanda vitatu tu vya kusafisha mafuta ghafi.
ChanzoBBCSwahili
0 maoni:
Post a Comment