Kesi inayomkabili
aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo na Charles Ble Goude inaanza
kusikilizwa leo katika mahakama ya jinai ya kimataifa mjini The Hague Uholanzi.
Wanakabiliwa na
mashataka ya madai ya kuhusika kwao kwenye vurugu za baada ya uchaguzi mkuu
nchini Ivory Coast mwaka wa 2011.
Wawili hao wanakanusha
mashtaka hayo. Wakati huo, Laurant Gbagbo alikuwa rais na Charles Ble Goud
akiwa kamanda wa kijeshi wa karibu.
Leo hii unatarajiwa
kutolewa uamuzi wa kesi hiyo iuliosubiriwa kwa takriban miaka mitatu ama minne
hivi.Laurent Gbagbo anatarajiwa kuonekana mahakamani , baada ya kutoa ombi la
kuachiliwa kwa muda ili kufuatia hali mbaya ya kiafya iliyokuwa inamkabili na
ombi hilo kukataliwa mnamo mwezi September mwaka wa jana.
Naye aliyekuwa mkuu
wake wa majeshi , Charles Ble Goude, atapanda mahakamani kukabiliana na
mashtaka yanayomkabili. Wote wawili wanatuhumiwa kwa makosa manne ya uhalifu
,mauaji,ubakaji,vitendo vya kinyama na mateso kwa binaadamu madai ambayo wote
wawili wameyakana.
Mahakama hiyo ya ICC
inaangalia zaidi ushahidi utakaotolewa wa waathirika wa matendo ya wawili hao
pindi walipokuwa mamlakani na inatarajiwa muwakilishi atafika mahakamani kupata
maamuzi ya mahakama mjini The Hague.
KUTOKA BBC
0 maoni:
Post a Comment