Watafiti nchini
Marekani wametoa onyo kuwa inaweza kuchukua miongo kadhaa ili kupatikana kwa
kinga ya virusi vya Zika kutengenezwa .Wanasayansi hao wa chuo kikuu cha Texas
kimesema kuwa muda mrefu hadi chanjo hiyo kupata idhini .
wanasema virusi vya mbu
hawa vinaweza kuleta majanga makubwa zaidi.Na suala hili limehusishwa na
madhara ya ubongo wakati mtoto akiwa tumboni.
Hata hivyo watafiti
nchini marekani wamelitaka shirika la afya duniani WHO kuchukua hatua ili
kukabiliana na usambaaji wa virusi vya
Zika,ambavyo vimesemekana kuwa ni athari
kubwa .
Raisi Barack Obama
ametaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kupata chanjo na tiba ya ugonjwa huo. msemaji
wa Ikulu ya white house,Josh Earnest,amesema kipaumbele cha serikali ya
marekali ni kutoa elimu kwa uma kuhusu athari ya ugonjwa huu.
Ernest anasema kwamba
"Tumejikita kwenye ushauri wa kisayansi uliopo ili kuwalinda wamarekani na
cha muhimu na kwanza kabisa tumeanza kwa kutoa tahadhari kwa watu kuhusu
mipango yao ya kusafiri kwa kuwa wanaweza kwenda eneo ambalo virusi vya ugonjwa
huu vipo.
Tunataka kuwa na
uhakika kuwa watu wanapata elimu ya kutosha kuhusu athari ya virusi hivi lakini
pia tunachukua kila hatua ili kutoa tahadhari ambazo ni muhimu kuchukuliwa ili
kupambana na ugonjwa huu."
CHANZO NI BBC
0 maoni:
Post a Comment