Man City imekua timu ya
pili kufuzu fainali ya mchezo wa kombe la Capital baada ya kuichapa Everton kwa
mabao 3-1.
Everton ndio walikua wa
kwanza kuzifuma nyavu za Man City baada ya kiungo Ross Barkley kuifungia timu
yake bao la kuongoza katika dakika ya 18 ya mchezo.
Kiungo kutoka Brazil
Fernandinho akasawazisha bao hilo kwa shuti kali baada ya kutoka piga nikupige
kwenye goli la everton katika dakika ya 25.
Kevin De Bruyne
akaongeza bao la pili baada ya kunganisha krosi ya kutoka upande wa kushoto
iliyopigwa na Raheem Sterling, kisha Sergio Aguero kun, akahitimisha kazi kwa
bao la tatu.
Katika mchezo wa kwanza
uliofanyika Goodson Park Everton walishindwa kwa ushindi wa mabao 2-1.
Man City watachuana na
Liverpool katika mchezo wa fainali utaofanyika Februari 28 katika dimba la
Wembley.
Mshirikishe mwenzak
0 maoni:
Post a Comment