Kwa mara ya kwanza
Umoja wa Mataifa umeweka wazi uraia wa wanajeshi wa kulinda amani wanaoshtumiwa
kuwa wamekuwa wakiwadhulumu watoto kingono Jamhuri ya Afrika ya kati.
Washukiwa hao ni raia
wa Bangladesh, the DRC, Niger na Senegal.
Akihutubia wanahabari
mjini New York, afisa mkuu wa UN Anthony Banbury karibu atokwe na machozi
wakati alipotangaza kesi za hivi karibuni za unyanyasaji wa kingono dhidi ya
watoto.
Mwezi ulopita, jopo
huru lilikashifu jibu la UN kuhusu madai hayo kama yenye makosa makubwa.
0 maoni:
Post a Comment