Meli ya kubwa
iliyoegemea upande mmoja inakaribia kufika katika pwani ya Ufaransa, maafisa wa
bahari wanasema, ingawa kuna matumaini ya kuiokoa kabla ya kuzama.
Meli hiyo kwa jina
Modern Express ambayo, imesajiliwa Panama, ilianza kulala upande mmoja Jumanne
baada ya kutokea kwa hitilafu za kimitambo.
Mabaharia wote 22
wameondolewa kutoka kwenye meli hiyo.
Juhudi za kuisimamisha
zimefeli, lakini maafisa wanasema jaribio jingine litafanywa leo Jumatatu.
Juhudi za leo
zikishindikana, basi meli hiyo itagonga pwani ya Ufaransa kati ya Jumatatu
usiku na Jumanne asubuhi.
Hali mbaya ya hewa
ilitatiza juhudi za uokoaji Jumapili.
Meli hiyo imebeba tani
3,600 za mbao na mashine kadha za uchimbaji, na imeinama kwa pembe ya kati ya
nyuzi 40 na 50.
Ina
tani 33 za mafuta
Mwaka 2002, meli ya
kusafirisha mafuta kwa jina Prestige ilizama karibu na pwani ya Uhispania na kumwaga
mafuta tani 50,000 na kuchafua eneo kubwa la bahari.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment