MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

NDEGE YA KIVITA YA UAE YATOWEKA YEMEN

UAE
Umoja wa Milki za Kirabau umesema ndege yake ya moja ya kivita imetoweka ikitekeleza mashambulio dhidi ya waasi wa Houthi nchini Yemen.

Shirika la habari la serikali ya nchi hiyo, WAM, lilitangaza kutoweka kwa ndege hiyo bila kutoa maelezo zaidi.

UAE imekuwa ikishiriki katika mashambulio ya muungano wa mataifa yanayoongozwa na Saudi Arabia kutekeleza mashambulio ya angani 
kumuunga mkono Rais Abedrabbo Mansour Hadi tangu Machi 2015.

Watu 6,000 wameauawa kwenye mapigano nchini Yemen.

Hicho ndicho kisa cha kwanza cha kutoweka kwa ndege ya UAE kwenye mapigano hayo.
Houthi
Maafisa bado hayajaeleza ndege iliyotoweka ni ya muundo gani na pia iwapo marubani walidhurika.

Jeshi la wanahewa la UAE hutumia ndege za kivita aina ya F-16 na Mirage 2000.

Desemba, ndege aina ya F-16 ya jeshi la Bahrain ilianguka Saudi Arabia kutokana na “hitilafu za kimitambo”, na mwezi Mei ndege ya kivita ya Morocco ilitunguliwa nchini Yemen.


Ndege hizo mbili zilikuwa zikishiriki mashambulio dhidi ya waasi wa Houthi.

kutoka BBC Swahili
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment