Rais Jacob Zuma wa
Afrika Kusini ameshtumiwa kwa kutoa matamshi yanayowabagua wanawake kijinsia.
Chama cha upinzani
nchini Afrika Kusini kinadai kuwa Zuma aliwadhalilisha waandishi wanawake juma
lililopita aliposema kuwa ni vigumu kwa wanaume siku hizi kuwatambua wanawake
warembo.
Nikisema kuwa wewe ni
mrembo katika ulimwengu huu wa wazungu unajitia katika hatari ya kushtakiwa kwa
kumdhalilisha mwanamke ''
Itakuwaje ?
''Zamani ningekueleza
'Gqezu, Gqezu ntomazane! Nongenazo izinkomo uyayidla inyama',"
Tafsiri ya Zulu kuwa
,''Japo sina mali ya kutosha ya kugharamia malipo ya mahari, naomba nikuoe''
jarida la News24 linamnukuu rais huyo.
''Kama mngeturuhusu
tuwatambue,bila shaka hata hawa walinzi wangu wangewaeleza jinsi mlivyo
warembo.''
''Lakini sikuhizi
thubutu, utashtakiwa hapa kwa kumdhulumu mwanamke wa wenyewe kijinsia''
''Mtawakosa wanaume
wazuri sana wenye nia ya kuwaoa eti kwa sababu ya haki zenu za msingi'' alisema
Zuma akicheka.
Yamkini Zuma,mwenye
wake 4 alitoa matamshi hayo akiambatana na mkewe, Tobeka Madiba Zuma,na mwanaye
mwenye umri wa miaka 8 katika hafla hiyo ya kuwahamasisha wapiga kura
kujiandikisha katika maeneo ya KwaZulu-Natal.
Msemaji wa chama cha
upinzani cha Democratic Alliance (DA) Phumzile Van Damme alituhumu Zuma kwa
matamshi hayo.
Kutoka BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment