Marekani imeitaka Urusi kuishinikiza Syria kusitisha kuvamia raia na
badala yake kuzingatia makubaliano ya kusitisha mapigano.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ametoa kauli hiyo baada ya
hospitali moja iliyopo kwenye eneo la waasi kushambuliwa kwa ndege huko mjini
Allepo, ambapo madaktari na watoto wameuawa.
Amesema Marekani imeshtushwa na shambulizi hilo ambalo limefanywa kwa
kukusudiwa.
Zaidi ya watu sitini wameuawa mjini Aleppo lakini kipindi cha saa
ishirini na nne zilizopita katika maeneo yanayohodhiwa na serikali pamoja na
waasi.
Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa amesema hali ni ya kusikitisha.
Msemaji wa ikulu ya Marekani Josh Earnest amezungumzia kuongezeka kwa
vurugu hizo
'' Tunalaani vikali wimbo jipya la mashambulizi ya anga ambayo
yamesababisha vifo vya zaidi ya watu sitini katika mji wa Aleppo katika kipindi
cha saa ishirini na nne pekee.
Tumeshangazwa zaidi na shambulizi la anga lilipofanywa katika hospitali
iliyopo mjini Aleppo ambalo limeuwa takriban wagonjwa kumi na nne na madaktari
watatu- akiwemo pamoja na daktari pekee wa watoto katika mji huo''.
Maeneo ya mji wa Aleppo yamekabiliwa na mashambulizi mapya kutoka
serikalini.
Wanaharakati wametoa picha za video zinazoonyesha waokoaji wanavyotafuta
watu waliosalimika katika tukio hilo.
0 maoni:
Post a Comment