Mkutano huo wa
kwanza wa viongozi na watu mashuhuri duniani ambao unajulikana kama mkutano wa
Giants Club utaongozwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Mkutano huo pia
utawashirikishia viongozi wa makundi ya uhifadhi wa wanyama, wafanyabiashara na
wanasayansi.
Kabla ya kufanyika
kwa mkutano huo, Rais Kenyatta amesema ametoa wito kwa hatua madhubuti
kuchukuliwa dhidi ya biashara haramu ya pembe.
Rais Kenyatta
amesema kuwa ndovu wanakabiliwa na hatari ya kuangamizwa na kizazi kipya cha
wawindaji haramu, waliojihami vilivo na walio na uhusiano wa kimataifa, na
matokeo yake yamekuwa mabaya sana.
Wataalamu wanasema
idadi ya ndovu Afrika ilishuka kwa asilimia 90 karne iliyopita na wanaonya kuwa
huenda wanyama hao wakaangamia katika miongo kadha ijayo.
0 maoni:
Post a Comment