Bei ya
mafuta imepanda hadi zaidi ya dola 50 kwa pipa kwa mara ya kwanza kabisa mwaka
huu mwaka 2016 wakati uzalishaji wa chini na kuongozeka kwa mahitaji ya mafuta
vikiendelea kuchangia kupanda kwa bei.
Kupanda
kwa bei ya mafuta kunafuatia takwimu za Marekani zinazoonyesha kushuka kwa
uzalishaji hasusan kutokana na moto nchini Canada.
Uzalishaji
wa mafuta yasiyosafishwa nchini Marekani ulishuka kwa pipa milioni 4.2 hadi
pipa milioni 537.1 kwa wiki kwa mujibu wa idara ya nishati nchini humo..
Canada
ndiye muuzaji mkubwa zaidi wa mafuta kwa Marekani na moto wa msituni katika
mikoa iliyo magharibi, ulisababisha kupungua kwa karibu mapipa milioni moja kwa
siku.
Mazungumzo
ya hivi majuzi kati ya nchi za Opec na Urusi kuhusu kupunguza uzalishaji wa
mafuta yamechangia kupanda kwa bei.
0 maoni:
Post a Comment