MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Arsene Wenger: Arsenal imesitisha mazungumzo na Sanchez na Ozil

Alexis Sanchez na Mesut OzilHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAlexis Sanchez alijiunga na Arsenal 2014, mwaka mmoja baada ya Mesut Ozil
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema klabu hiyo imesitisha kwa muda mazungumzo kuhusu mikataba ya Alexis Sanchez na Mesut Ozil hadi mwisho wa msimu.
Mshambuliaji wa Chile Sanchez na kiungo wa kati wa Ujerumani Ozil, wote wenye umri wa miaka 28, wamesalia na chini ya miaka miwili kwenye mikataba yao.
Wenger amesema tayari amefanya uamuzi wake kuhusu mustakabali wake Arsenal, lakini bado hajatia saini mkataba wa miaka miwili aliopewa na klabu hiyo.
"Kwa sasa hatujaafikiana," Wenger alisema kumhusu Sanchez.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment