MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Bunge la Uingereza latoa idhini kujitoa umoja wa Ulaya

Kifungu namba 50 cha katiba kinampa mamlaka waziri mkuu kuitisha mchakato huo
Image captionKifungu namba 50 cha katiba kinampa mamlaka waziri mkuu kuitisha mchakato huo
Bunge la Uingereza limetoa idhini ya mwisho ya sheria muhimu katika hatua ya mchakato wa kuelekea kutaka kujitoa katika jumuiya ya Ulaya.
Serikali ya Uingereza inapanga kuanza hatua rasmi za kujiondoa ndani ya jumuiya ya Ulaya ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.
Hatua hii inatarajiwa kuwa na utata kufuatia tangazo la Scotland linalodai kuwa wanampango pia wa kuwa na kura ya maoni kuhusiana na kujitenga kwao na Uingereza na kisha kuwa taifa huru.
Aidha Waziri mkuu kwa mjibu wa kifungu namba 50 kinampa uwezo kuitisha mchakato huo mapema zaidi kuanzia siku ya leo jumanne.
Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya bunge la Uingereza zinasema kuwa hakuna uwezekano wa mchakato huo kuanza wiki hii na kwamba Waziri mkuu atatakiwa kusubiri hadi mwisho wa mwezi huu muda ambao ni rasmi.
Chama upinzani cha Liberal kimesema kuwa serikali imeshindwa kuonyesha msimamo juu ya haki za raia wa EU wanaoishi nchini Uingereza na kutoa wito kwa makundi mbali mbali kusisitiza juu ya mabadiliko.

Kutoka BBC Swahili
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment