ARSENAL YATOKEA TUNDU YA SINDANO
Kocha wa Arsene Wenger, amekiri kuwa ushindi wao wa mabao 7-5 dhidi ya Reading siku ya Jumanne usiku, wakati wa mchuano wa kombe la Ligi uliwanusuru kutoka kwa maangazi makubwa.
Amesema amefurahishwa sana na jinsi wachezaji wake walivyojitahidi wakati wa mechi hiyo kwa kutoka nyuma ya kufungwa mabao 4-0 kufikia wakati wa mapunziko.
Katika kipindi cha pili Arsenal, ilifunga mabao manne hatua iliyopelekea mechi hiyo kuongezwa muda wa ziada.
Theo Walcott alifunga mabao matatu naye Marouane Chamakh alifunga mawili na kusaidia Arsenal kufuzu kwa raundi ya tatu.
"Tulitoka kwenye wimbi la aibu na kuibuka na ushindi ambao haukutarajiwa na zaidi ya yote heshima na hadhi miongoni mwa mashabiki wetu ambao walikuwa wamekata tamaa" alisema Wenger.
Kocha wa Reading Brian McDermott, amesema matokeo hayo ndio mabaya zaidi tangu alipoanza kazi ukufunzi.
Baada ya dakika 35, Arsenal tayari ilikuwa imelazwa mabao manne lakini Walcott aliifunguia Arsenal bao lake la kwanza muda mfupi kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Lakini baada ya dakika Tisini za mechi kumazika, timu hizo mbili zilikuwa zikitoshana nguvu ya mabao 4-4

0 maoni:
Post a Comment