Ripoti
za mahakama nchini Burkina Faso zinasema kuwa mwili ambao unakisiwa kuwa wa
raisi wa zamani aliyeuawa Thomas Sankara utafukuliwa hii leo katika jaribio la
kutaka kubainisha ikiwa ni wake...........
Familia
na marafiki wa rais Sankara wamekuwa na shauku iwapo mabaki hayo ni yake.
Bwana
Sankara aliuawa wakati wa mapinduzi mwaka 1987.
Sankara
alichukuwa uongozi baada ya mapinduzi ya mwaka wa 1983.
Sankara
alipinduliwa na Blaise Compaore ambaye aliitawala Burkina Faso hadi mwaka
uliopita alipolazimishwa kuondoka na maandamano makubwa katika mji mkuu wa wa
nchi hiyo Ouagadougou.
Madaktari
wawili kutoka Burkina Faso na mmoja kutoka Ufaransa watachukua chembechembe za
mwili huo na kuipima wakitumia mashine na mbinu za kisasa za DNA ilikubaini
kikamilifu iwapo inahusiana na mwili wa Sankara.
Miili
mingine 12 ya wafuasi wake waliouawa pamoja naye pia itafukuliwa.
Mabaki
hayo ya Sankara yamezikwa katika makaburi ya Dagnoen katika mji mkuu wa
Ouagadougou.
Familia
yake inashuku kuwa huenda mwili huo sio wake.
CHANZO BBC
0 maoni:
Post a Comment