Uongozi
wa serikali mpya ya rais Muhamadu Buhari ambayo itaingia madarakani siku ya
ijumaa wiki hii inaulaumu utawala unaondoka wa Goodluck Jonathan kwa kuhujumu
taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.........
Uongozi
wa All Progressives Congress (APC) unailaumu utawala uliopoa sasa kwa ukosefu
mkubwa wa mafuta ukosefu wa umeme na upungufu wa uzalishaji kutokana na migomo
inayoendelea ya wafanyikazi na deni kubwa la taifa.
APC
inailaumu PDP kwa kuiwacha taifa hilo katika hali mbaya ya kiuchumi na hivyo
kuhujumu utawala unaotarajiwa kushika hatamu karibuni.
Kwa
mujibu wa msemaji wa APC Lai Mohammed,''hii ndiyo mara ya kwanza katika
historia ya taifa hilo kwa serikali kupeana mamlaka huku uchumi ukiwa katika
hali mabaya zaid''
''Kwa
sasa uchumi wetu ambao ndio mkubwa zaidi barani Afrika unadeni kubwa la dola
milioni 60 nao wafanyikazi wamegoma wakidai mabilioni ya fedha.
''Umeme
haupo na mafuta pia ambayo ndio nguzo ya uchumi haipo kwa kweli uchumi
umekwama''aliongezea Lai.
Kwa
upande wache chama cha rais anayeondoka Goodluck Jonathan PDP kimekanusha madai
ya kuhujumu uchumi wa Nigeria.
Msemaji
wa rais Goodluck Reuben Abati,aliwashukuru wanigeria kwa kumpa fursa ya
kuwaongoza .
Kupitia
kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter alituma ujumbe kwa niaba ya rais Goodluck
ambaye alihudhuria misa yake ya mwisho akiwa rais na akawaaga wafuasi wao.
MM MMsemaji
wa chama chake Olisa Metuh naye aliwaonya wanachama wa chama cha Buhari kukoma
kuichafulia jina chama cha PDP.
BwanaZSZ Metuh alisema si kweli kuwa PDP kimehujumu uongozi na uchumi wa Nigeria
''
Imekuwaje kuwa katika utawala wa rais Goodluck hakujatokea ukosefu kama huu wa
mafuta na umeme ''?
''Nahisi
kama kuna watu wenye ushawishi katika serikali inayokuja ambao wanataka kuzua
hali ya taharuki na kuibua madai kuwa hawakurithi kitu chochote katika akiba ya
serikali''.
Mwandishi
wa BBC aliyeko Nigeria anasema kuwa chanzo cha uhaba huo mkubwa wa mafuta na
umeme ni mashirika na makampuni yanayoagiza mafuta ambayo yameamua kususia
kuingiza mafuta yakidai malimbikizo ya pesa wanazodai serikali.
Jenerali
mstaafu Buhari alishinda uchaguzi wa urais wa Nigeria katika uchaguzi
uliofanyika tarehe 28 mwezi Machi na kuipa chama cha upinzani ushindi wake wa
kwanza katika historia ya taifa hilo.
Buhari
ameratibiwa kuchukua uongozi wa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta
ijumaa ijayo.
Majuzi
kampuni zinazotoa huduma za simu zilitangaza kuwa zimelazimika kutumia mafuta
kuzalisha umeme hatua ambayo ni ghali na kuwa hazingemudu gharama zake.
Nigeria
ambayo huzalisha takriban mapipa milioni mbili ya mafuta kila siku haina vinu
vya kusafishia mafuta nchini humo na inalazimika kuagiza mafuta kutoka nje.
KUTOKA BBC
0 maoni:
Post a Comment