Raia wanne wa Rwanda wameambia BBC kwamba walilazimishwa
na jeshi la nchi hiyo kujiunga na waasi wa M23 Mashariki mwa Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Wanne hao wamesema walitoroka mapigano
na kwamba wanajaribu kuomba hifadhi katika nchi jirani ya Uganda.
Mmoja wa Wanyarwanda hao wamesema asili
mia 90 ya wapiganaji wa M23 ni wanajeshi wa Rwanda.
Mwenzake ambaye ni mwanafunzi wa utabibu
amesema amewahudumia wapiganaji 300 waliojeruhiwa kwa risasi.
Serikali ya Rwanda imekanusha kuunga
mkono waasi wa M23. Msemaji wa jeshi la Rwanda Joseph Nzabamwita amesema wanne
hao wanatumia kisingizio cha kulazimishwa jeshini ili kupata hifadhi.
Kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment