Geoffrey Mutai bingwa wa mbio za Kilomita 21 za New York |
Bingwa Mtetezi wa mbio za New
York Marathon Geoffrey Mutai
alitoka nyuma na kuthibitisha udedea wake katika barabara za mji huo wa
Marekani alipokata utepe akitumia muda wa saa moja na sekunde hamsini..........
Muingereza Mo Farah, hata hivyo, ndiye aliyewaduwaza
mashabiki wake nchini Marekani alipokunguwaa na kuanguka baada ya takriban
kilomita tisa na kisha akajifua na kurejea kwa kishindombio zikikaribia
kukamilika .
Bingwa huyo wa mbio za mita elfu tano na mita elfu
kumi za olimpiki alimaliza katika nafasi ya pili sekunde 18 pekee nyuma ya
Mkenya mshikilizi wa muda bora katika mbio za marathon duniani.
Farah alishikwa na kisunzi punde baada ya kukamilisha
mbio hizo na alilazimika kubebwa kwa machela.
Mo Farah azirahi baada ya kukamilisha mbio za New York
|
Muingereza huyo baadaye alisema alikuwa sawa na kuwa
ataendelea na mazoezi yake kabla ya kushiriki mbio zake za kwanza za marathon
katika mashindano ya London Marathon
zitakazoandaliwa mwezi ujao.
0 maoni:
Post a Comment