Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, limetangaza kufanya
maandamano makubwa siku ya Jumatatu ya Machi 17, endapo Manispaa ya Ilala
itashindwa kuwajibu ombi lao la kuongezewa heka 11 katika eneo la Jangwani ili
wajenge Uwanja wa kisasa wa michezo..............
Maandamano hayo yatashirikisha wanachama na wapenzi wa
Yanga, kwa madai kuwa serikali imeshindwa kuwathamini na kutotambua mchango
wao, licha ya klabu hiyo kujihusisha na mambo mengi ya kimaendeleo.
“Tunatoa siku tano tano za serikali kwa kupitia Manispaa ya Ilala, chini ya Meya wake Jerry Silaa kujibu maombi
Uongozi wa Yanga kupitia Katibu mkuu wake Bw-Benny
Njovu, umeitisha maandamano mach 17, mwaka huu siku a Jumatatu, na kumtaka kamanda wa Polisi kanda maalum ya DSM, Seleman Kova, kutoa Kibali cha maandamano
hayo.
Barua hiyo
ilisema kuwa uamuzi wa kuitisha maandamano hayo umetokana na Manispaa ya Ilala
kuchelewesha maombi yao ya kuongezewa eneo la ujenzi wa Uwanja, hivyo wao
wameamua kuandamana kisheria.
Lakini alipotafutwa Kova, kuzungumzia swala hilo
alisema kuwa yeye hakuwepo ofisini, hivyo hana jibu lolote juu ya maandamano
hayo.
“Nipo nje ya Ofisi kwa siku nzima ya leo (jana), hivyo
sijui lolote juu ya madai hayo,” alisema Kova.
0 maoni:
Post a Comment