Mcheza filamu wa Hollywood,Harrison Ford,
anapatiwa matibabu katika Hospitali moja mjini Los Angels baada ya ndege yake
kuukuu kuanguka katika uwanja wa Gofu..............
Mcheza
filamu huyo mwenye umri wa miaka 72 alikuwa akiendesha ndege hiyo mwenyewe.
Ndege
hiyo ndogo ilinasa kwenye mti wakati ilipokuwa ikitua kwa dharula.
Mashuhuda
wa ajali hiyo wamesema Harrison Ford alikuwa amejeruhiwa, akionekana kuwa na
damu iliyotapakaa usoni.
Matabibu
wamesema Ford anaendelea vizuri na kuwa hali yake itatengemaa kabisa.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment