MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

SUDAN KUSINI WALIBAKA NA KULA WATU:AU

Muungano wa Afrika umeilaumu jeshi la serikali ya Sudan Kusini na vikosi vya waasi kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na uhalifu wa kivita.

Uchunguzi wa AU ulibaini kuwa mapigano yaliyotokea mwezi Disemba mwaka 2013 yalitokana na mzozo kati ya makabila ya Dinka na Nuer ndani ya kikosi cha kumlinda rais.

Aidha uchunguzi huo umebaini kuwa vikosi hivyo hasimu viliwachinja watu na kuwalazimisha watu waliodhaniwa kuwa mahasimu wao kula nyama ya binadamu na kunywa damu yao.
Jopo hilo la uchunguzi chini ya aliyekuwa rais wa Nigeria Olusegun 
Obasanjo limepata majina ya watu wanaodhaniwa kuwa walioendesha 
kampeini hizo za ubakaji wa wanawake na ulaji wa watu.

Ripoti hiyo imeorodhesha matukio ya utekaji na udhalilishwaji wa wanawake.

Aidha majina ya watu waliotekeleza matukio hayo imebainika kuwa ni ya raia ambao hawakuwa wakishiriki vita vyenyewe.

Matukio mabaya zaidi yaliripotiwa katika miji ya Juba, Bor, Bentiu na Malakal.
Watu kadhaa walioshuhudia mwanzo wa vita hivyo mjini Juba wanasema kuwa walilazimishwa kunywa damu ya watu ambao ndio walikuwa wameuawa.

Makaburi ya halaiki pia yalifichuliwa katika uchunguzi huo ulioendeshwa tangu mwaka jana jopo hilo la uchunguzi lilipoundwa.

Maelfu ya watu wameripotiwa kufariki tangu kuanza kwa vita hivyo yapata miaka miwili.

Watu zaidi ya milioni mbili wamelazimika kutoroka makwao na kuwa wakimbizi wa ndani kwa ndani.
Jopo hilo limependekeza watu waliotajwa wafikishwe katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyoundwa na muungano huo wa Afrika.

Licha ya hofu ya kuwa maelfu ya watu wa kabila fulani walilengwa na kuuawa jopo hilo linasema kuwa Hakukuwa na ushahidi uliopatikana wa kuthibitisha kuwa kulifanyika mauaji ya kimbari.

KUTOKA BBC.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment