Ray Tomlinson, raia wa
Marekani, ambaye ndiye aliyevumbua utumaji wa barua pepe kwa Kiingereza e-mail
amefariki dunia.
Tomlinson amefariki
akiwa na umri wa miaka 74.
Mgunduzi huyu aliibuka
na wazo la kutuma ujumbe wa kieletroniki kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia
mitandao mbali mbali mwaka 1971.
Aliandika ujumbe wa
kwanza wa barua pepe wakati akifanya kazi Boston, kama Mhandisi wa kompyuta.
Pia alikuwa mwanzilishi
wa matumizi ya alama "at"(@)kuwa ndio alama kuu ya utumaji wa barua
pepe.
Wakati wa uhai wake
Tomlinson alisema hawezi kukumbuka barua pepe yake ya kwanza ilielezea nini.
chanzo BBC Swahil
0 maoni:
Post a Comment