Korea Kaskazini
imetishia kutekeleza mashambulio ya nyuklia dhidi ya Korea Kusini na Marekani
iwapo nchi hizo mbili zitaendelea na mazoezi ya pamoja ya kijeshi.
Mazoezi hayo, ambayo
hufanyika kila mwaka, mwaka huu yatashirikisha wanajeshi 300,000.
Serikali ya Korea
Kaskazini imetoa taarifa ya ikitishia kutekeleza “shambulio la nyuklia kwa
ajili ya haki”.
Ni kawaida kwa
Pyongyang kutoa vitisho vya aina hiyo na wataalamu wanatilia shaka uwezo wa
Korea Kaskazini kuwa na makombora ya nyuklia.
Hisia hupanda kati ya
Korea Kaskazini na Korea Kusini na Marekani kila mazoezi hayo ya pamoja ya
kijeshi yanapofanyika.
Pyongyang hutazama
mazoezi hayo kama mazoezi ya kujiandaa kuivamia
Kutoka BBC Swahili.
0 maoni:
Post a Comment