Mgombea urais
anayeongoza katika kinyang’anyiro cha kumteua mgombea wa chama cha Democratic
Hillary Clinton amekataa kushiriki mdahalo wan ne dhidi ya mpinzani wake Bernie
Sanders.
Maafisa wake wa kampeni
wamesema badala yake, Bi Clinton ameonelea ni heri kukabiliana na mgombea
mtarajiwa wa chama cha Republican Donald Trump.
Bi Clinton alikuwa
awali amekubali kushiriki mdahalo wa mwisho kabla ya mchujo muhimu katika jimbo
la California na katika majimbo mengine matano wiki mbili zijazo.
Bw Sanders, Seneta wa
Vermont, amesema hajashangazwa na uamuzi huo wa mpinzani wake.
BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment