BEI YA VYAKULA YAPANDA DUNIANI
Bei ya vyakula duniani ilipanda kwa asilimia kumi mwenzi
Julai na kusababisha hofu ya kupanda kwa bei ya vyakula
Barani Afrika.
Taarifa hii ni kwamujibu wa ripoti iliyotolewa na benki ya
Dunia.
Ripoti hiyo inasema kuwa wimbi la joto lililoikumba Marekani
Pamoja na ukame katika baadhi ya maeneo ya mashariki mwa
Ulaya ndiyo chanzo kikubwa cha kupanda kwa bei hizo.
Bei ya nafaka kama vile mahindi, ngano, na maharage ndiyo
Ilipanda sana kulingana na ripoti hiyo.
Benki hiyo imeonya kuwa nchi ambazo hununua nafaka kutoka
Nje ndizo zitakazo athirika sana.


0 maoni:
Post a Comment