WAkENYA 48 WAUAWA
Polisi nchini Kenya, wanasema kuwa watu 48 waliuawa usiku wa
kuamkia leo kufuatia mapigano makali kati ya jamii za Pokomo
na Orma katika eneo la Mto Tana kusini mashariki mwa KENYA.
Mauaji hayo yalitokea wakati watu wenye silaha kutoka jamii ya
Pokomo waliposhambulia kijiji kimoja katika eneo la Reketa huku
Wakiteketeza makazi ya watu.
Naibu kamanda wa polisi mjini Mombasa, Joseph Kitur, amethibitisha
Kuwa watu 48 waliuawa ,31 kati yao ni wanawake, watoto 11 na wanaume 6.

0 maoni:
Post a Comment