Marekani na Umoja wa Ulaya
wamewataka viongozi wa Sudan Kusini kuendeleza hali ya utulivu na kuzuia
vitendo vya ghasia baada ya Rais Salva Kiir kulivunja baraza la mawaziri
akiwemo naibu wake.
Rais wa Sudani kusini |
Marekani imesema imesikitishwa sana
na hali ya kuhatarisha utulivu wa taifa hilo changa duniani.
Bwana Kiir alilivunja baraza la
mawaziri siku mbili zilizopita katika kile kinachoonekana kuwa ni kugombea
madaraka kati yake na makamu wa rais Riek Machar.
Sudan Kusini yenye utajiri mkubwa wa
mafuta ilipata uhuru wake kutoka Sudan mwaka 2011 baada ya miaka mingi ya
mgogoro kati ya nchi mbili hizo.
Vikundi mbalimbali vyenye silaha
vimeendeleza harakati zao nchini humo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya
Sudan Kusini Mayek Makol amesema Rais Kiir anafanya mashauriano akipanga kuunda
serikali mpya.
Hata hivyo amekataa kusema
mashauriano hayo yatachukua muda gani.
"huenda yakachukua siku tatu,
nne, au wiki moja", amesema.
Kwa wakati huu wafanyakazi
waandamizi wa umma, wanaendesha shughuli za serikali ya nchi hiyo ambayo ni ya
mwisho kwa maendeleo duniani.
Katika taarifa yake, wizara ya mambo
ya nje ya Marekani imesema:" Ni muhimu kwa Sudan Kusini kubaki na mtazamo
wake wa ukweli iliouonyesha wakati wa siku ya uhuru wake miaka miwili
iliyopita."
Zaidi ya watu milioni 1.5 waliuawa
na wengine zaidi ya milioni nne kukosa mahali pa kuishi wakati wa mgogoro kati
ya Sudan Kusini, ambako watu wengi ni Wakristo au kufuata imani za dini za
kimila, na waislam wenye kuzungumza Kiarabu , Sudan kaskazini.
Lakini nchi hiyo imepata matatizo
sugu ya kiuchumi tangu wakati huo na kuimarika kwa uchumi wake kumecheleweshwa
na mvutano juu ya mpaka na mafuta kati yake na majirani zao Sudan Khartoum.
Mabomba ya mafuta huko sudani kusin |
0 maoni:
Post a Comment