Mjukuu wa rapper na muigizaji Ice-T amekamatwa na polisi
wiki iliiyopita baada ya kumfyatulia risasi kwa bahati mbaya rafiki yake
anaeishi nae chumba kimoja............
Kwa mujibu TMZ, polisi waliuambaia mtandao huo kuwa
kijana huyo anaefahamika kwa jina la Elyjah Marrow alikuwa ameshikilia bunduki
katika chumba chake huko Georgia na bahati mbaya risasi ikafyatuka na kumpiga
rafiki yake, Daryus Johson mwenye miaka 19.
Kwa mujibu wa polisi, walipofika katika eneo la tukio
walimkuta kijana huyo na baada ya kumpekuwa walipata madawa ya kulevya aina ya
marijuana ambayo alikuwa na nia ya kuyauza.
Kijana huyo amefunguliwa mashitaka ya kuua bila
kukusidia, kukutwa na bangi na kumiliki bunduki ambayo ilitajwa kuwa ya wizi.
Marrow aliwahi kuonekana kwenye reality show ya Ice
Cube, “Ice Loves Coco.”
0 maoni:
Post a Comment